HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumapili, 6 Mei 2018

SIMBA SC YA POPADIC WATU WALIKUWA WANASTAREHE KWA SOKA SAFI NA USHINDI MNONO

Kocha wa Simba SC, Mserbia Dragan Popadic akizungumza na kiungo aliyekuwa anaweza kucheza kama beki pia, Mwanamtwa Mussa Kihwelo kabla ya moja ya mechi za timu hiyo mwaka 1995 Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru mjini Dar es Salaam  
Popadic aliiwezesha Simba kutwaa mataji saba kati ya mwaka 1994 na 1996, mawili ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, sasa Kombe la Kagame miaka 1995 na 1996, ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo, 1994 na 1995, ubingwa wa Ligi ya Muungano mwaka 1994 na ubingwa wa Kombe la Nyerere miaka ya 1994 na 1995. 
Popadic aliingia Simba akichukua nafasi ya kocha mzawa, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ aliyekuwa akisaidiwa na Mhabeshi, Entenneh Eshenteh ambao kwa pamoja waliifikisha timu hiyo Fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993.