Msanii wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize ameingia Tena Kwenye vita ya maneno na Ex girlfriend wake staa wa Bongo movie Jacqueline Wolper.
Tangu jana kumekuwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii zilizomuonyesha Wolper akimrushia Dongo Sarah ambaye ni mpenzi wa Harmonize kwa kumuita Mlezi wa wana baada ya taarifa kusambaa kuwa kamtosa Harmonize na kumchukua Mwarabu Fighter.
Baada ya dongo hilo la Wolper, Harmonize alitokwa na povu zito kwani kwa Kupitia ukurasa wake wa Instagram alimtetea mpenzi wake Sarah na kusema yeye sio Mlezi wa wana ila Wolper ndo Mlezi wa Wana na kuambatanisha na listi kamili ya wanaume wote aliokuwa nao Kwenye Mahusiano