HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Ijumaa, 25 Mei 2018

Jangwani sasa Maisha Matamu

Baada ya Shirikisho la soka Barani Afrika CAF kulipa sehemu ya kitita cha Mil 600, viongozi wa Yanga wamemaliza madai ya wachezaji, imefahamika.

Yanga imetimiza ahadi yake ya kuweka kipaumbele kwa wachezaji kwa kulipa malimbikizo yao ya mishahara.

Ahadi hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wake Charles Mkwasa wakati ikisaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa na baadae kombe la Shirikisho kwa kusema pesa watakazolipwa na CAF sehemu kubwa itatumika kumaliza madai ya wachezaji.

Yanga sasa inamaliza michezo miwili ya ligi iliyobaki huku morali ya wachezaji wake ikiwa juu baada ya kuwa wamejaa 'mapesa'.

Baada ya kumaliza mchezo wa mwisho dhidi ya Azam FC Jumatatu, May 28 kikosi cha Yanga kitaelekea nchini Kenya kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup.

Yanga pia imekusudia kwenda Nairobi kufanya vizuri na ikiwezekana kutwaa taji hilo ambalo bingwa atajinyakulia kitita cha Tsh Mil 68 pia kusafiri nchini Uingereza kucheza na Everton.