
Golikipa wa klabu ya Yanga Sc Ramadhan Kabwili ameachwa ndani ya kikosi cha Timu ya Taifa U20 maarufu kama NgorongoroHeroes kwa kile kilichodaiwa kuwa ana majukumu kunako kikosi cha Yanga.
Ufafanuzi wa taarifa hii ni kutokana na golikipa wa Yanga Sc Beno Kakolanya kuwa majeruhi hivyo Yanga hawawezi kusafiri na golikipa mmoja tuu kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wao wa kombe la shirikisho barani Afrika ikiwa ni hatua ya makundi.
Kwa mujibu wa kocha wa kikosi cha NgorongoroHeroes Ammy Ninje amesema atamchukua Golikipa wa Jku ya Zanzibar ili kuziba nafasi hiyo.
Ikumbukwe Ramadhan Kabwili ndiye Golikipa aliyepata jina kubwa kutokana na ushujaa wake kunako michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika chini ya miaka 17 akiwa na kikosi cha Serengeti Boys ndipo akasajiliwa Yanga Sc.
Ili usipitwe na habari kama hizi kiurahisi ungana nasi kupitia instagram@sokaonline