Kikosi cha Yanga kinapaa kesho Alhamisi kwenda nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza kundi D kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya USM Alger.
Mchezo huo utapigwa Jumapili usiku, May 06 2018 huko nchini Algeria.
Idadi kubwa ya mashabiki wamejiandikisha kusafiri na kikosi cha Yanga ambacho kinaondoka mapema kesho kupitia Dubai.
Gharama ya safari hiyo ni dola 732, kwenda na kurudi.
Yanga itaondoka Algeria May 07 kurejea nchini.
Mashabiki waliojitokeza kusafiri na timu kwenda kuiunga mkono nchini Algeria wameonyesha umuhimu wa kila shabiki wa kweli kuwa na timu yake katika mazingira yote.
Katika mchezo huo wa ugenini Yanga inahitaji hata matokeo ya sare kama itashindwa kuibuka na ushindi.
Uhamasishaji mkubwa unapaswa kufanywa hapa nyumbani ili kuhakikisha Yanga inashinda michezo yote mitatu itakayopigwa kwenye uwanja wa taifa.
Michuano hii ya CAF ndio kipaumbele cha Yanga sasa hasa baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Simba na kufifisha matumaini ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo