HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Alhamisi, 3 Mei 2018

Maelekezo ya Waziri wa Afya kuhusu kitendo cha Mbunge ‘kumchoma’ sindano Mwanafunzi

Baada ya picha ya Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga kusambaa kwenye mitandao ya kijamii akimchoma sindano mwanafunzi kama ishara ya kuzindua chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi wilayani Ulanga, Waziri wa Afya, Manendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto ameibuka na kusema kuwa kitendi hicho si sahihi.

Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo baada ya watumiaji mbalimbali wa mitandao ya kijamii kulaani kitendo hicho huku baada wakisema ni kucheza na afya za watu, kutokana na mtu asiye na utaalamu wa kitabibu kifanya shughuli hiyo.

Waziri Mwalimu amesema kuwa, amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya atoe maelekezo ili kuhakikisha kuwa, kanuni za kitabibu zinazingatiwa.

“Hii sio sahihi. Tayari nimeshamuelekeza Katibu Mkuu Afya kutoa maelekezo mara moja kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusisitiza uzingatiwaji wa Miongozo ya Utoaji wa Huduma za Afya nchini. masuala ya kitaalamu yafanywe na Wataalamu.”

Hapa chini ni baadhi ya waliotoa maoni yao katika ukurasa wetu wa Twitter.