Ajali hiyo ilitokea jana usiku wakati wakitokea kwenye maadhimisho ya Mei Mosi wilayani Newala.
Mtwara. Msemaji wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Mtwara (Mtwarefa), Juma Mohamed amethibitisha kotokea kwa ajali iliyowahusisha wachezaji wa timu ya Mwena FC ya Ndanda wilayani Masasi.
Mohamed amesema ajali hiyo ilitokea jana usiku wakati wakitokea kwenye maadhimisho ya Mei Mosi wilayani Newala.
Amesema watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha na kwamba taarifa za kina zitatolewa baadaye mchana.