HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Ijumaa, 25 Mei 2018

MO RASHID NAYE HUYOOO MSIMBAZI


KATIKA kuhakikisha wanaimarisha safu ya ushambuliaji kwa kujiongezea idadi kubwa ya mabao msimu ujao, uongozi wa Simba upo katika mchakato wa kumsajili straika wa Tanzania Prisons, Mohammed Rashid `Mo Rashid`, akitarajiwa kuanza vitu vyake katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, itakayoanza mwishoni mwa mwaka huu.

Mo Rashid ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kutakiwa Msimbazi ili kuiongezea nguvu safu ya ushambuliaji, yenye nyota kama Emmanuel Okwi na John Bocco.

Msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Mo Rashid amefunga mabao 10, huku Okwi akicheka na nyavu mara 20 na Bocco 14, wakati Marcel Boniveture wa Majimaji, ambaye alitua Dar es Salaam jana kumalizana na Simba, akiwa na mabao 13, hali inayoweza kukifanya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao kuwa moto wa kuotea mbali msimu ujao.

Akizungumza na BINGWA Dar es Salaam jana, Samwel Sango, ambaye ni Meneja wa Mo Rashid, alisema amepokea ofa kutoka timu mbili ambazo ni Simba na Singida United, kuhitaji huduma ya mteja wake huyo.

Alisema Simba wameweka mezani dau la Sh milioni 25, huku meneja huyo akishindwa kuanika dau la Singida United.

“(Mo Rashid) amemaliza mkataba na Prisons, kwa sasa ni mchezaji huru, viongozi wa Simba nimeongea nao na kutaja ofa hiyo, lakini kwa thamani ya Mo Rashid, si hiyo waliyotaka wao. Pia Singida nao wamekuja, lakini wote wanatakiwa kuongeza dau,” alisema.

BINGWA lilimtafuta Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah `Try Again` kuzungumzia usajili wa mchezaji huyo, ambapo alisema hawezi kusema lolote, kwani bado hawajapokea ripoti kutoka kwa kocha wao, Pierre Lechantre.

“Kwa sasa ni mapema sana, bado hatujapokea ripoti kutoka kwa kocha, hali hiyo hatuwezi kusajili, kwani tunaweza kumsajili mchezaji hali ya kuwa si mapendekezo ya benchi la ufundi,” alisema Try Again.

Mo Rashid aliwahi kuingia mkataba wa awali wa mwaka mmoja na Yanga kipindi cha dirisha dogo la usajili, lakini uongozi wa timu hiyo uliachana naye baada ya kugundua nyota huyo bado ana mkataba na Prisons.