-Mwalimu wa shule ya upili alifichua alichofanyiwa na mwanafunzi wake
-Mwalimu huyo mrembo alipata barua ya mapenzi kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wake aliyekiri kuzinguliwa na urembo wake
-Chioma ni mwalimu ambaye hana mume na anaishi eneo la Nnewi, Anambra
Mwanafunzi wa kiume wa shule moja ya upili alifichua penzi lake kwa mwalimu wake bila kujali yale ambayo yangemwandama.
Mwalimu huyo kwa jina Chioma U. Jane alifichua jinsi mwanafunzi huyo alivyomwandikia barua akisema urembo wake ulimzingua sana.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Chioma anayefunza shule moja ya upili eneo la Nnewi, Anambra nchini Nigeria alikuwa akipanga dawati lake ofisini alipopata barua ya mwanafunzi wake akieleza jinsi alivyoenzi urembo wake.
Mwalimu huyo alipachika barua hiyo ya mwanafunzi wake kwenye mtandao wa kijamii na kuwashangaza mashabiki wake kutokana na ujasiri wa mwanafunzi wake.
Habari Nyingine: Tabia 5 za wanawake za kushangaza kanisani
Barua ya mwanafunzi huyo ilisema,“Shangazi Chioma,
Hili linaweza kuwa sio kawaida lakini ninamaanisha kila kitu ninachokisema. Kutoka siku ya kwanza nilipokuona, akili yangu ilisimama. Kila ninapokuona, ni kama moshi inatokea kwenye macho yangu. Nina matumaini ya kuwa mtu tajiri. Ninajua utasema mimi ni kijana mdogo, lakini wacha nikwambie ukipenda mtu, umri haujalishi. Ninapoteza udhabiti wangu kila mara ninapokuwaza. Ninapofunga macho yangu, ninakuona. Tafadhali, wazia ombi langu na unifae angalau mara moja.
Mimi wako mpenzi,
Pin Code.”
Mwalimu mmoja wa shule ya upili nchini Chioma U. Jane amefichua barua ambayo aliandikiwa na mwanafunzi wake ambaye alidai kuwa urembo wake ulimzingua. Picha: Facebook/ Beautiful Pictures
Malimwengu!