Kumekuwa na maneno ya chini chini mtaani kuhusiana na ishu ya wasanii wa muziki Tanzania kwamba wamekuwa wakifanya kila njia kutengeneza idadi kubwa ya views katika video zao ili kupata kick na kutengeneza pesa. Kikubwa inasemwa kwamba wasanii hao wapo tayari hata kununua viewers ili tu waonekane wamefanya kazi bora. Kuhusu hilo msikie Alikiba.
Akiwa na ‘hit song’ ya ‘Mvumo wa Radi’ ambayo ni #1 trending video Youtube Alikiba maarufu kama King Kiba amefunguka na kudai yeye sio miongoni mwa wasanii wanaotegemea kupata pesa kutoka katika ‘views’ za Youtube kama baadhi yao wanavyofikilia vichwani mwao.
King Kiba ametoa kauli hiyo ikiwa zimepita siku kadhaa tokea Youtube account ipoteze uwezo kuendelea kuhesabu idadi ya watu walioitazama video yake mpya ‘Mvumo wa Radi’, jambo ambalo wengi wao walidai kuna mchezo anafanyiwa msanii huyo ili asiweze kufikisha ‘views’ wengi kama ilivyokuwa kawaida yake kila atowapo video.
“Hii ndio mara ya kwanza kunitokea tatizo hilo ila halijaweza kuniathiri kwa namna yeyote ile.
“Ila nashukuru watu wamepata walichokuwa wanastahili nasio kwamba mimi nategemea pesa kutoka ‘Youtube views’, mimi nafanya muziki najua wapi napata pesa katika muziki wangu.
“Nilichokuwa nahitaji kiukweli ni mashabiki zangu waridhike na waelewe mimi ni msanii wa aina gani”, amesema Alikiba.
Pamoja na hayo, Alikiba ameendelea kwa kusema “tunajua kwamba kuna hizi biashara za kuweka ma-robot katika ‘Youtube’ ili ionekane watu wana ‘view’ kwa wingi ila mimi binafsi ninaona ni utoto tu. Haitokuja kutokea hata siku moja kwamba Alikiba ameweka ‘robot’ ili apate ‘views’ nyingi, mimi nafanya muziki wangu kwa ajili ya watu na kwanini sasa nidanganye watu”
Wimbo wa Alikiba kwa sasa umetazamwa na jumla ya watu milioni 1.2 na kushikilia nafasi ya kwanza katika ya video zilizotazamwa kwa kiasi kikubwa kutoka Youtube.