Mwanaume mmoja, raia wa India ambaye anafanya biashara ya mboga za majani ameripotiwa kujiua Mei 10, 2018 baada ya kupokea bili ya umeme ya gharama ya Dola za Marekani 13,000 sawa na Shilingi za Kitanzania milioni 31.2.
Mwanaume huyo anayefahamika kwa jina la Jagannath Shelke, 36, alikuwa ni mkazi wa kusini mwa Maharashtra nchini humo.
Familia yake imeliambia Shirika la Utangazaji BBC kuwa Jagannathaliacha ujumbe kuwa amejiua kutokana na bili hiyo ya umeme kuwa kubwa sana.
Hatahivyo inaelezwa kuwa bili hiyo ilikuwa imekosewa, bili sahihi ilikuwa ni Dola za Marekani 41.6 sawa na takriban Shilingi za Kitanzania 98,000.