Aliyekuwa Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady amesema alimpenda sana muimbaji huyo na kila mtu alifahamu hilo ila dharau zilizidi, ndipo akaamua kuvunja mahusiano yao.
Zari katika mahojiano na Kiss FM nchini Kenya amesema kwa kawaida mwanaume anaweza kuchepuka ila kwa Diamond dharau zilizidi na alihisi kama utu wake umeshushwa.
Ameendelea kwa kusema kuwa Diamond alikuwa akimkosea heshima katika mitandao ya kijamii na hakuwa na heshima kwa wanawake kitu kilichopelekea hata watoto wake kutukanwa na ukizingatia hawana baba hivyo hakuona sababu ya kuendelea na mahusiano hayo.
“I loved diamond so much. God blessed us with two beautiful kids. But I decided to leave because he kept disrespecting me.
"When a man keeps disrespecting you, it’s time to move on. Diamond kept on repeating the same mistakes he had done. I kept asking myself ‘why do I have to settle for less?’. I then decided to call it quits.
"When you get insults from trolls, even your kids feel it as well. I have all grown boys and couldn’t stay anymore. For the sake of the children, I think it was the right time to go. I ‘m raising my sons to respect women."- Zari
February 14 mwaka huu Zari alitangaza kuvunja rasmi mahusiano yake na Diamond Platnumz. Kwa sasa Zari yupo nchini Kenya kwa ajili ya event yake ‘The Colour Purple’ itakayofanyika weekend hii Uhuru Gardens.