Mhilu ana nafasi kubwa ya kuongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo inawakosa nyota muhimu na wenye uzoefu ambao hawakusafiri na timu kuja Algeria kutokana na sababu mbalimbali.
PATA HABARI KWA HARAKA ZAIDI KWENYE SIMU YAKO Download katisha blog App👇👇Bonyeza hapa👇👇https://play.google.com/store/apps/details?id=com.katisha.blog BLOG APP
Algers, Algeria. Mshambuliaji chipukizi wa Yanga, Yussuf Mhilu amepanga kutumia kukosekana kwa washambuliaji tegemeo wa timu yake kwenye mechi dhidi ya USM Alger kesho usiku kama fursa ya kujiuza kwa mawakala wa soka ili apate nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania.
Mhilu ana nafasi kubwa ya kuongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo inawakosa nyota muhimu na wenye uzoefu ambao hawakusafiri na timu kuja Algeria kutokana na sababu mbalimbali.
Wachezaji hao ambao wameshindwa kuambatana na timu Algeria ni Obrey Chirwa, Donald Ngoma, Amissi Tambwe ambao ni majeruhi huku Ibrahim Ajibu akikosekana kutokana na matatizo binafsi.
"Nadhani kila mchezaji ana lengo la kucheza soka la kulipwa na unapofika hatua kama hii uwezekano wa kutimiza lengo hilo unakuwa ni mkubwa kwa sababu mawakala wanakuwa wanafuatilia kila mechi.
Hivyo mechi ngumu kama hizi ndio naamini natakiwa kuonyesha kiwango bora zaidi ili kuisaidia timu yangu kupata matokeo, pia ili niweze kujiuza,"alisema Mhilu.
Kinda huyo ana uwezekano mkubwa wa kupata nafasi ya kuanza kwenye mchezo huo kama mshambuliaji wa kati akiwa sambamba na ama Juma Mahadh au Rafael Daud ambao hata hivyo sio washambuliaji asilia.
Ukiondoa Mhilu, mshambuliaji asilia aliyepo kwenye msafara wa Yanga huku Algeria ni Yohana Nkomola ambaye hata hivyo ndio ameanza kurejea uwanjani baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha.
PATA HABARI KWA HARAKA ZAIDI KWENYE SIMU YAKO Download katisha blog App👇👇Bonyeza hapa👇👇https://play.google.com/store/apps/details?id=com.katisha.blog BLOG APP