HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 1 Mei 2018

Petroli na dizeli zashuka bei. Bei mpya hizi hapa


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei elekezi za mafuta zitakazoanza kutumia kuanzia keshi Mei 2, 2018.

Katika taarifa ya EWURA, bei za rejareja za mafuta ya petroli zimepungua kwa TZS 88 kwa lita moja, dizeli imepungua kwa TZS 61 kwa lita moja, huku mafuta ya taa yakipanda kwa TZS 2 kwa lita moja.

Aidha kwa upande wa bei za jumla, bei za mafuta yote zimepungua ambapo petroli imepungua kwa TZS 100.91 kwa lita moja, dizeli TZS 73.71 kwa lita na mafuta ya taa TZS 10.49 kwa lita moja.

Hapa chini ni bei elekezi zilizotolewa na EWURA;

Download