Dodoma. Hoja tano ambazo Spika Job Ndugai alizisimamia bungeni zimesababisha aanze kuangaliwa kwa mtazamo tofauti na wabunge na wananchi wengine.
Awali kulikuwa na mitazamo hasi dhidi ya kiongozi huyo wa moja ya mihili ya nchi na mijadala ilitawala, hususan katika mitandao ya kijamii kwamba anakifanya chombo hicho kutofanya vizuri kazi yake ya kuisimamia Serikali, lakini misimamo yake ya hivi karibuni itawafanya wenye fikra hizo wafikirie tofauti.
Hivi sasa katika mitandao ya kijamii, hasa Facebook na Instragramu kumejaa video zinazomuonyesha akiwabana mawaziri au Serikali katika masuala kadhaa.
Hoja hizo zilizogeuza upepo ni; suala la uhaba wa mafuta ya kula na sukari, kamatakamata inayofanywa na polisi dhidi ya bodaboda, kutaifishwa kwa mifugo, kutowalipa wakulima fedha zao na ushuru wa mauzo ya nje ya korosho (export levy) na Operesheni ya Sangara, 2018.
Wabunge hao wanaendelea kusema Spika Ndugai anapaswa kuusimamia ipasavyo mhimili huo ili Serikali iogope na kutekeleza yale ambayo yanapitishwa kwa ajili ya utekelezaji.
Mawaziri walioonja ‘kibano’ cha Spika Ndugai ni Dk Philip Mpango (Fedha na Mipango), Charles Mwijage (Viwanda, Biashara na Uwekezaji), Luhanga Mpina (Mifungo na Uvuvi) na Dk Hamisi Kigwangalla wa Maliasili na Utalii.
Mbali na hao, Spika Ndugai akitoboa siri ya Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba kumwaga machozi kama mtoto mdogo alipofika mbele ya kamati ya bajeti.
“Huyu ndiye Ndugai aliyekuwa kipindi anachaguliwa,” alisema mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Kabwe Zitto wakati Mwananchi lilipotaka maoni yake kuhusu msimamo alioonyesha Ndugai katika siku za karibuni.
“Kwamba Job Ndugai ni mtu mwenye msimamo na asiyeyumba siku zote tangu amekuwa mbunge, mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili, mwenyekiti wa Bunge, Naibu Spika na sasa Spika.
“Hapa katikati hatukuelewana kidogo (lakini) sasa amekuwa yeye. Huyu mnayemwona ndiye Ndugai mwenyewe.”
Zitto ambaye pia ni kiongozi wa ACT-Wazalendo alisema Ndugai anatimiza wajibu wake wa kikatiba kama spika na anapaswa kuuungwa mkono licha ya kutokubaliana naye kwenye baadhi ya mambo.
Zitto anaungwa mkono na mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia ambaye anasema kutofuata utaratibu uliowekwa ni fujo.
“Mkuu wa mhimili akisimamia utaratibu muhimili utakuwa sawa na kwa sasa amejaa kwenye kiti chake kama Spika,” alisema Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.
“Kazi ya Bunge ni kuisimamia na kuishauri Serikali, kwa hiyo anachokifanya Spika ni kuisaidia nchi na historia itamkumbuka.”
Mbatia alisema kinachofanywa na Spika Ndugai kinapaswa pia kufanywa na waliopo chini yake kama Naibu Spika, Dk Tulia Ackson na wenyeviti wa Bunge.
Lakini mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea anaona si rahisi kumuamini Ndugai hadi mwisho.
“Anaweza kuwa na jambo zuri lenye maslahi ya Taifa, (lakini) likaishia kusikojulikana,” alisema Kubenea.
“Hajafikisha hata robo ya (Spika wa Bunge la Tisa, (Samuel) Sitta au nusu ya (Spika wa Bunge la Kumi, Anne) Makinda. Anataka kuonyesha anaweza kusimamia Bunge, basi asimame kama walivyofanya Sitta na Makinda.”
Kubenea alisema huku nyuma Bunge lilikuwa linasimama lenyewe kama mhimili unaojitegemea badala ya kusimama chini ya miguu ya Serikali na kupangiwa baadhi ya mambo.
“Bado hajanivutia ingawa ni kweli kuna mabadiliko eneo fulani anaonekana anayafanya. Anachopaswa kukifanya ni kusimama kama Spika wa Bunge, muhimili unaojitegemea,” alisema Kubenea
Mbunge huyo alisema tangu mkutano wa Bunge la bajeti ulipoanza Aprili 3, wabunge wamekuwa wakilalamikia kitendo cha Serikali kutotoa fedha zinazopitishwa na Bunge jambo linaloonyesha muhimili huo unadharaulika.
“Bunge linatenga bajeti lakini fedha haziendi. Haya ni matatizo ambayo msingi wake mkuu ni Bunge,” alisema Kubenea.
“Huko nyuma Serikali ilikuwa inaliogopa Bunge. Kwa hiyo Spika Ndugai anapaswa kusimamia hili ili Bunge litekeleze wajibu wake wa kuisimamia na kuishauri Serikali.”
Mkazi wa jijini Dodoma, John Frank alisema ingawa hawawezi kuona moja kwa moja mikutano ya Bunge, kile wanachokiona kwa kutumia simu kuwa Spika amekuwa mbogo, kinaonyesha kuna mabadiliko.
“Nafikiri Spika ameona imebaki kama miaka miwili na zaidi muda wake kumalizika, sasa anaamua kusimama na kuonyesha ule umwamba wake wa kipindi kile cha Escrow ili naye akiondoka aweze kukumbukwa. Ndivyo ninavyofikiri mimi.”
Mei 24, Spika Ndugai alitoboa siri ya kile kilichompata Waziri Tizeba mbele ya kamati ya bajeti, akisema “alilia kama mtoto mdogo”, lakini akaigeuzia kibao Wizara ya Fedha akiitaka itathmini utendaji wake.
Kauli hiyo aliitoa baada ya mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye kutaka shughuli za Bunge ziahirishwe ili kujadili jambo la dharura lililohusu fedha za ushuru wa mauzo ya nje ya korosho (export levy).
Nape alifikia uamuzi huo baada ya suala hilo kupelekwa kamati ya bajeti Mei 16 na mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu lakini alisema walipofika huko hawakuelewana kwani Serikali haikutoa majibu yanayoridhisha.
“Haya ni mambo yanasikitisha sana. Mara ya mwisho waziri wetu wa kilimo alipokwenda kwenye kamati ya bajeti, ilibidi atoe machozi. Amelia kama mtoto mdogo,” alisema Spika Ndugai.
“Watu wanalaumiwa, mtu analaumiwa, wala sio mkosaji. Wizara ya Fedha kuna mambo yanakwenda huko, sisi tunakuwa hatujui. Kwa hiyo tunawaona kama ninyi wabaya.
“Hivi kwa nini ukae na hela ya mtu, awe anakuomba, anakupigia magoti, anakulambalamba na hela ni yake. Hapa tulipofika mbali sana. Sasa waheshimiwa mawaziri wawe wanalia kweli kwenye kamati za Bunge? Kweli? Hapana, hapana, wizara ya fedha hebu mjitathimini.”
Katika tukio jingine Mei 24, Spika alimbana Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba akisema suala la bodaboda kukamatwa na polisi na kuwekwa vituo vya polisi, linapaswa kuangaliwa kwa kuwa zipo nyingi na inahitajika kufanyika sensa ili kuangalia jinsi vijana wanavyopoteza mali zao kwa kukamatwa na polisi katika maeneo mbalimbali katika makosa madogo tu
Alisema Serikali inapoteza fedha nyingi kupitia kwa waendesha bodaboda. Alitoa mfano wa kituo kikuu cha polisi cha mkoa wa Dodoma ambako alisema kuna pikipiki zaidi ya 300 zilizokamatwa bila ya kuwepo makosa makubwa.
Awali, Dk Mwigulu aliagiza bodaboda ambazo zinashikiliwa na polisi kwa makosa madogo ziachiwe mara moja na wahusika wapewe nafasi ya kwenda kutafuta faini wakiwa na vyombo vyao.
“Naagiza kuanzia leo (Mei 24) na nitapita kuangalia maeneo mbalimbali pikipiki ambazo hazihitajiki kwenda mahakamani kwa ajili ya kutolea ushahidi nataka ziachiwe mara moja ili kuwapatia wenye mali,” alisema Mwigulu.
Spika Ndugai alifikia hatua hiyo baada ya mbunge wa Mpwapwa (CCM), George Lubeleje kuomba mwongozo kwa kuhusu kamatakamata ya waendesha bodaboda inayofanywa na Jeshi la Polisi.
Lubeleje alisema pikipiki zinaozea vituo vya polisi na kwamba polisi wamekosa huruma kwa vijana wa Tanzania na kuomba waruhusiwe kutumia pikipiki hizo kutafuta faini wanazodaiwa na polisi.
Pia Mei 22, wakati Bunge likiwa limekaa kama kamati ya matumizi kupitia bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, suala la uwekeji vigingi kwa maeneno yanayopakana na hifadhi, liliibuka na wabunge kutaka lisitishwe.
Walikuwa wanaungana na maoni ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu uwekaji uwekaji huo wa vigigi.
Spika Ndugai aliunga mkono maoni ya kamati baada ya mbunge wa Serengeti (Chadema), Ryoba Chacha kukamata shilingi ya mshahara wa waziri akitaka maelezo ya kina ili kazi hiyo isitishwe, hoja iliyojadiliwa na wabunge waliodai majibu ya waziri hayakuridhisha.
Spika alisema tatizo la watu wa hifadhi ni ulafi wa ardhi, lakini uhusiano baina ya wananchi na hifadhi huko chini na kuhoji kwa nini hivi sasa umetoweka.
“Ushauri uliotolewa na kamati naona ni mzuri tu. Kabla ya kuweka vigingi mshauriane kwanza na kukubaliana,” alisema Ndugai.
“Lakini hili sijui la kuweka vigingi halafu baadaye uje usogeze sidhani kama ni sawa. (Hifadhi za Taifa za Tanzania) Tanapa hili linawezekana kweli, yaani muweke vingingi halafu siku mje mvitoe? Hapana.”
Mei 18, Spika Ndugai akiongoza kamati ya matuzi, alilizungumzia suala lililoibua karibu siku mbili za majadala wa bajeti ya wizara ya mifugo na uvuvi la operesheni sangara ambao wabunge walidai imekuwa ikitumia ubabe, vitisho na ukiukwaji wa haki za binadamu ambapo walitaka kamati iundwe kwenda kuchunguza.
Spika Ndugai alimtaka Waziri Mpina kufungua masikio yake yote kusikia kila kitu na kukifanyia kazi kwani endapo itaundwa kamati itakwenda kubaini madudu mengi ambayo anaweza kuyafanyia kazi kwa kuchukua ushauri wa wabunge.
102
Chukia
Sura ‘mpya’ ya Spika Job Ndugai
mwananchi.co.tz
May 27, 2018 8:40 AM