HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 8 Mei 2018

Timu sita hatihati kushuka daraja

Timu zilizokalia kuti kavu ni pamoja na Mbeya City, Kagera Sugar, Majimaji, Mbao FC, Ndanda na Njombe Mji.

Dar es Salaam. Timu sita za zipo katika hatihati ya kushuka daraja mpaka Ligi Daraja la Kwanza endapo zitashindwa kuzichanga karata zao vizuri katika mechi zilizosalia.

Timu zilizokalia kuti kavu ni pamoja na Mbeya City, Kagera Sugar, Majimaji, Mbao FC, Ndanda na Njombe Mji.

Katika msimu huu wa ligi wenye timu 16, kati ya hizo mbili ndiyo zinatakiwa kushuka daraja na kubaki 14 ambazo zitaungana na timu sita zilizopanda daraja na kuwa 20 zitakazocheza msimu ujao.

Njombe, Ndanda na Mbao ndiyo zina hatari kubwa zaidi ya kushuka kutokana na kuwa na pointi chache.  Njombe wanashika mkia wakiwa na pointi 22, Ndanda ni ya pili kutoka mwisho na pointi 23 wote wakizipata kwenye mechi 27 walizocheza.

Kocha mkuu wa Njombe Mji, Ally Bushiri alisema, bado wana nafasi ya kubaki Ligi Kuu licha ya kikosi chake kinashika mkia: "Lolote linaweza kutoka na mechi zetu zilizobaki ndiyo zinazoweza kuamua safari hiyo ya kubaki au kushuka daraja."

Hata hivyo, historia ya ligi za nyuma inaonyesha kuwa timu ambazo zilifanikiwa kufikisha pointi 30 na zaidi, huwa zinanusurika na janga hilo.