HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumapili, 6 Mei 2018

TIRA IKISHIRIKIANA NA TAASISI YA BIMA NCHINI IIT YAZINDUA MFUMO WA TIIP

Kamishna wa Bima nchini, Dkt. Baghayo A. Saqware akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo mara baada ya kuzindua mfumo wa kieletroniki ujulikanayo kama Tanzania Imports Insurance Portal(TIIP)utakao wezesha waagizaji bidhaa nje ya nchi kununua Bima toka kampuni za kitanzania,mfumo huo umeandaliwa na TIRA ikishirikiana na Taasisi ya Bima nchini (IIT)warsha iliyofanyika juzi jijini Arusha na kuhudhuriwa na wadau wa Bima.(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha)

Meneja wa kanda kaskazini wa usimamizi mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Elieza Rweikiza akizungumza katika mafunzo hayo jijini Arusha Juzi

Wadau wa Bima wakisikiliza kwa makini

Mkurugenzi wa Leseni na Usimamizi wa Mwenendo wa Soko Samwel Mwiru akifafanua jambo kwa waandishi wa habari ambapo pamojana mambo mengine alisema kuwa Soko la bima Tanzania linaendeshwa na kampuni za bima zipatazo 31,madalali takribani 150 na wakala wa bima wapatao 413,Sekta ya bima husimamiwa na Mamlaka ya usimamizi wa bima (TIRA)kwa mujibu wa sheria ya bima ya mwaka 2009

Rais wa Taasisi ya Bima Tanzania BoscoJames Bugali akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha.