HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 19 Mei 2018

Ulinzi wa kihistoria mechi ya Simba vs Kagera sugar Taifa - Sports Kitaa

Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli akisubiriwa kuikabidhi Simba Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu, ulinzi wa aina yake umewekwa uwanjani hapa.
Tofauti na siku za kawaida ambapo usalama uwanjani hapa usamiwa na Jeshi la Polisi, zoezi hilo leo linaongozwa na Idara ya Usalama wa Taifa ambayo imekuwa ikiratibu na kusimamia kila kinachoendelea.
Sehemu ya geti kubwa la kuingilia Uwanja wa Taifa, limejaa maofisa wa usalama wa Taifa ambao wamekuwa wakiruhusu magari machache yenye ruhusa maalum kuingia uwanjani huku mengi yakitakiwa kupaki nje ya uwanja.
Askari Polisi na wale wa kikosi cha Ulinzi cha Jeshi la Kujenga Taifa (Suma JKT) wamekuwa mbali na geti hilo na wamesambazwa nje ya uwanja ambako kuna makundi ya mashabiki wanaokata tiketi na wale wanaoingia uwanjani.

Askari hao Polisi leo ndio wamekuwa wakitii maagizo wanayopewa na Maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa tofauti na siku za kawaida ambapo wao ndio huwa wakisimamia shughuli za usalama.

Katika kuhakikisha ulinzi upo imara uwanjani hapa, Helkopta ya Jeshi la Polisi imekuwa ikifanya doria katika maeneo yanayozunguka uwanja wa Taifa