HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 5 Mei 2018

VIDEO: Mkongo wa Yanga hakuna kulala Algeria


Yanga itaanza mechi zake za hatua ya makundi kesho dhidi ya USM Alger, wakiwa Kundi D pamoja na Gor Mahia na Rayon Sports
Algiers, Algeria. Kama wachezaji wa Yanga walidhani watakula bata mara baada ya kuondoka kwa George Lwandamina basi wanajidanganya kwani kocha wao mpya Mwinyi Zahera ameonyesha yeye ni mtu wa kazi pengine kuzidi Mzambia huyo.
PATA HABARI KWA  HARAKA ZAIDI KWENYE SIMU YAKO Download katisha blog App👇👇Bonyeza hapa👇👇https://play.google.com/store/apps/details?id=com.katisha.blog BLOG APP

Zahera licha ya urafiki na uchangamfu wake kwa wachezaji na viongozi wa Yanga, ameonyesha hataki mchezo linapokuja suala la kazi yake kutokana na jinsi anavyoweza kusimamia misimamo yake.
Katika kudhihirisha hilo, wachezaji wa Yanga walijijuta wakionja joto la jiwe siku ya kwanza tu walipowasili hapa Algeria baada ya kocha huyo kuwagomea ombi lao la kutofanya mazoezi ili wapumzike kumaliza uchovu wa safari.
Baada ya kutumia zaidi ya saa 20 safarini, wachezaji wa Yanga waliomba wasifanye mazoezi jana Ijumaa ili wapumzike kumaliza uchovu wa safari ombi ambalo ni kama lilikuwa kujipalia makaa mbele ya kocha huyo.
Zahera baada ya kusikia ombi hilo, aliwagomea wachezaji na kuwataka wapumzike kwa saa mbili tu kisha waanze kujiandaa kwenda mazoezini tofauti na matarajio hayo.
"Ilikuwa ni lazima wafanye mazoezi ili miili yao ifunguke na ukizingatia hali ya hewa ya huku ni baridi hivyo miili haipaswi kulala," alisema Zahera
PATA HABARI KWA  HARAKA ZAIDI KWENYE SIMU YAKO Download katisha blog App👇👇Bonyeza hapa👇👇https://play.google.com/store/apps/details?id=com.katisha.blog BLOG APP