HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 5 Mei 2018

Nkomola ugua, ila fiti kuivaa USM Alger

Daktari wa Yanga asema yupo fiti kucheza mechi ya Jumapili

Algiers, Algeria. Mshambuliaji chipukizi wa Yanga, Yohana Nkomola amefuzu vipimo vya afya na yuko tayari kuikabili USM Alger kesho saa 4:00 Usiku.
Muda mfupi baada ya Yanga kutua Algeria, mshambuliaji huyo aliugua ghafla jambo lililolazimu awahishwe hospitali alipatiwa matibabu na afya yake kurudi katika hali ya kawaida.
Daktari wa timu hiyo, Edward Bavu alisema maumivu ya mwili ambayo Nkomola aliyapata ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa tatizo ambalo kwa sasa halipo baada ya matibabu.
"Siyo tatizo kubwa. Tayari ameshafanyiwa matibabu na yuko fiti kucheza mechi Jumapili. Nadhani mabadiliko ya hali ya hewa ndio yamechangia ukizingatia tumetoka Tanzania ambako kuna joto kuja huku kwenye baridi hivyo kuna miili mingine haiwezi kukabiliana na mabadiliko hayo kwa haraka," alisema Bavu.
PATA HABARI KWA  HARAKA ZAIDI KWENYE SIMU YAKO Download katisha blog App👇👇Bonyeza hapa👇👇https://play.google.com/store/apps/details?id=com.katisha.blog BLOG APP