Kikosi cha Yanga kipo ugenini mjini Shinyanga kucheza mechi yake ya kukamilisha ratiba dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa CCM kambarage.
Yanga inapigania nafasi ya pili na Azam FC, ikiwa na rekodi ambayo si rafiki ya kupoteza michezo mitatu iliyopita kwenye ligi na jumla ikiwa ni nane bila kupata matokeo.
Katika mchezo wa mwisho wa ligi Yanga ilifungwa kwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kuelekea mchezo huo baadhi ya wachezaji wake nyota watakosekana ikwemo Papy Tshishimbi aliyesafiri kwenda kwao Congo kutibiwa, Ibrahim Ajibu anayemuuguza mkewe na Donald Ngoma aliye majeruhi kwa muda mrefu.
Mechi hiyo ya kukamilisha ratiba itaanza majira ya saa 10 kamili jioni