HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Alhamisi, 3 Mei 2018

Yanga wawafuata Waarabu na rekodi


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, wanaondoka nchini leo kuelekea Algeria kuwafuata wenyeji wao, USM Alger huku wakijivunia rekodi ya kiwango chao ugenini, lakini kubwa zaidi wakieleza kusahau kichapo kutoka kwa watani zao,

Simba na sasa wanaenda kusaka ushindi, ili kuianza vyema hatua hiyo ya makundi.Jumapili, USM Alger itaikaribisha Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, katika mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, alisema jana kuwa amewataka wachezaji wake kusahau matokeo ya mechi za ligi na kuanza safari mpya ya kupeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano hayo ya kimataifa wanayoshiriki.

Nsajigwa alisema anafahamu mechi za hatua ya makundi ni ngumu, lakini kuanza ugenini kutawasaidia kusaka ushindi baada ya kuwa na rekodi nzuri ya kuonyesha kiwango cha juu wanapokuwa nje ya ardhi ya nyumbani.

Yanga ambayo mwaka juzi ikiwa chini ya Mholanzi, Hans van der Pluijm ilifika hatua hiyo, imepangwa Kundi D pamoja na Rayon Sports ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya na USM Alger.

Baada ya kurejea nchini, Yanga itaendelea na mechi zake za viporo vya Ligi Kuu Bara ikiwamo cha Mtibwa Sugar na dhidi ya Mbao FC ambayo awali ilipangwa kuchezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.