HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 19 Mei 2018

Yanga yafunguka kumkosa Zahera



IKIWA bila ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera, kikosi cha Yanga kinatarajia kushuka kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga kucheza dhidi ya wenyeji Mwadui FC katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni ya kuendelea kukamilisha ratiba.

kocha Mkuu, Mwinyi Zahera.

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, alisema kuwa kocha Zahera ataendelea kukaa jukwaani kwa kuwa bado taratibu za ajira hazijakamilika.

Mkwasa alisema bado kocha huyo hajapewa mkataba wa ajira na klabu hiyo inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa kwa sababu  uongozi unaendelea kumfanyia tathmini.

"Unajua hata CAF jina la kocha ambalo lipo kule ni la George Lwandamina, hatujabadilisha, uongozi bado haujamalizana na kocha huyu (Zahera) na pindi mambo yatakapokaa sawa ataanza rasmi majukumu yake," alisema Mkwasa.

Aliongeza kuwa katika mchezo wa leo na mechi nyingine za ligi zilizobakia, benchi la ufundi litakuwa ni ya Kocha Msaidizi, Shadrack Nsajigwa.

"Kama uongozi zipo taratibu tunazozifanya na Wana-Yanga hawana haja ya kuwa na hofu, muda utakapofika na mambo yatakapokaa sawa kocha atakaa kwenye benchi na kuanza kuiongoza timu," Mkwasa aliongeza.

Yanga walivuliwa ubingwa Mei 10 mwaka huu baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 na watani zao Simba kutangazwa rasmi mabingwa wapya wa msimu huu wa mwaka 2017/18.

Mechi nyingine ya ligi hiyo inayotarajiwa kuchezwa leo ni kati ya mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC ambao wataikaribisha Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya kwenye Uwanja wa Azam Complex.