HOUSE OF ENTERTAINMENT

JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumapili, 6 Mei 2018

Yanga yaibuka na mbinu mpya

Nyota hao wanaamini, kama Yanga watapigana kiume na kupata pointi hizo hakuna uwezekano wa kuzuiliwa kuingia robo fainali, hatua ambayo itawafanya kuvuna pesa za maana kutoka Shirikisho la Soka Afrika (Caf).
JESHI la Yanga limetua salama jijini Algeria tayari kuwakabili wapinzani wao, USM Alger hapo kesho Jumapili, lakini wachezaji wake wameitazama vizuri ratiba ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kisha wakapiga hesabu rahisi ya kukusanya pointi 10 kwenye mechi nne za kwanza ili kuhakikisha wanafuzu hatua ya robo fainali.
Nyota hao wanaamini, kama Yanga watapigana kiume na kupata pointi hizo hakuna uwezekano wa kuzuiliwa kuingia robo fainali, hatua ambayo itawafanya kuvuna pesa za maana kutoka Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

PATA HABARI KWA  HARAKA ZAIDI Download katisha blog App👇👇Bonyeza hapa👇👇
Download katisha blog App👇👇Bonyeza hapa👇👇
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.katisha.blog

Beki wa pembeni wa Yanga, Juma Abdul alisema hawataki kuona wanaishia hatua ya makundi kama ilivyotokea misimu miwili iliyopita ambazo walifuzu kwenye hatua hiyo hivyo, wanataka kuvunja rekodi na kwenda mbele ili waandike historia mpya.
“Tumekuja huku Algeria kwa kazi moja tu ambayo ni kusaka pointi iwe kwa kupata ushindi au hata sare ili tujiweke nafasi nzuri ya kupata pointi 10 ambazo naamini tutaingia robo fainali.
PATA HABARI KWA  HARAKA ZAIDI Download katisha blog App👇👇Bonyeza hapa👇👇
Download katisha blog App👇👇Bonyeza hapa👇👇
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.katisha.blog
“Unajua mashindano kama haya jambo muhimu ni kupata ushindi katika mechi zote za nyumbani na ugenini hutakiwi kupoteza angalau upate hata pointi moja.
“Naamini tunaweza kupambana na kupata pointi jambo ambalo litakuwa chachu kwetu kupata ushindi katika mechi zetu mbili zinazofuata dhidi ya Rayon Sports na Gor Mahia,” alisema beki huyo wa kulia.
Yanga ilitua jijini Algiers jana Ijumaa saa 6.55 mchana ikitokea Dubai ambako iliunganisha ndege, ambapo kesho Jumapili usiku itashuka uwanjani. Baada ya mchezo huo, Yanga itarudi nyumbani kuikabili Rayon Sports. Baada ya hapo Yanga itaikaribisha Gor Mahia ambayo itarejeana nayo siku kumi baadaye, kisha itaialika USM Alger jijini na itafunga mahesabu ugenini Rwanda ambako itavaana na Rayon Sports mwezi Agosti.