Klabu ya Yanga na Donald Ngoma tayari wamefikia makubaliano ya kuvunja mkataba. Ngoma ambaye alikuwa amebakiwa na mkataba wa mwaka mmoja wamekaa na kukubaliana kuvunja mkataba uliobaki.
Donald Ngoma amekubali kuvunja mkataba wake ndani ya Yanga kwa sharti la kulipwa mshahara wa miezi 3 milioni 27 kama mkataba unavyosema na klabu ya Yanga imekubali kumlipa mshahara wa miezi mitatu ili kuachana naye.
Donald Ngoma amekuwa na majeruhi ya muda mrefu bila kupona na msimu huu Ngoma ameichezea Yanga mechi nne tu za ligi kuu Tanzania Bara na hajacheza tena mechi yoyote amekuwa nje akiuguza majereha yake.
Pia klabu ya Yanga imeachana rasmi na Beki Mkongo Festo Kayembe ambaye alisajiliwa katika dirisha dogo ila hajawahi kuichezea klabu ya Yanga katika mechi za mashindano rasmi zaidi ya kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na KMC tu.
Festo alisajiliwa kutoka kwao Congo kama mchezaji huru ila klabu aliyokuwa anaichezea SM Sanga Balende iligoma kutoa ITC ikidai Festo aliondoka klabuni hapo wakati hajamaliza mkataba wake ndio SM Sanga Balende wakaomba fedha za kufidia mkataba wake ndani ya klabu hiyo.
-Kwa sasa Yanga wanapanga kusajili wachezaji wawili wa kimataifa ili kuisaidia klabu hiyo kwenye michuano ya Afrika kinachosubiliwa na kocha mkuu wa klabu hiyo Mwinyi Zahera kupitisha usajili huo ili kamati ya Usajili iweze kukamilisha usajili huo.