HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 1 Mei 2018

YONDANI AZUIA ‘SUB’ YA TSHISHIMBI


globalpublishers.co.tz

PRESHA ya mchezo inaweza kukufanya ukafanya maamuzi ambayo ni magumu, ndivyo ilivyokuwa baada ya nahodha wa Yanga, Kelvin Yondani kuonekana akizuia mabadiliko ya kumtoa kiungo, Papy Tshishimbi katika mchezo wa jana dhidi ya Simba.

Tukio hilo lilitokea kipindi cha pili baada ya Simba kuwa mbele kwa bao 1-0 huku Yanga wakiwa pungufu kutokana na beki Has­san Kessy kupewa kadi nyekundu, ndipo benchi la ufundi likawa linataka kumtoa Tshishimbi la­kini Yondani akaelekea kwenye benchi na kuonekana akitoa ushauri wa kutofanya hivyo.

Licha ya ushauri huo bado Tshishimbi alitolewa katika dakika ya 80 na nafasi yake kuchukuliwa na Emmanuel Martin lakini hiyo haikuchan­gia kubadilisha matokeo ya mchezo huo ambapo Simba ilishinda bao 1-0.