Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ametaka kukutana na wachezaji wote wa Yanga jijini Dar es salaam, imefahamika
Zahera yupo Dar kwa siku kadhaa sasa ikielezwa anashirikiana na uongozi wa Yanga kukamilisha masuala ya usajili.
Kocha huyo ndiye anayetoa maamuzi ya mwisho kuhusu wachezaji wapya wanaosajiliwa lakini pia ndiye anayeamua ni wachezaji gani wabaki kwa ajili ya msimu ujao.
Baada ya kumalizika kwa michuano ya SportPesa Super Cup, wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko ya siku kadhaa kabla ya kurejea kuanza maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho.