HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 4 Juni 2018

BONGE la surprise mkutano wq Yanga



BONGE la surprise limeandaliwa na viongozi wa Yanga, kuelekea kwenye mkutano mkuu uliopangwa kufanyika Mei 10, mwaka huu, katika ukumbi utakaotajwa baadaye.


Mkutano huo ulipangwa kufanyika Juni 17 na baadaye kurudishwa nyuma kwa madai kuwa tarehe hiyo huenda ikagongana na Sikukuu ya Eid el Fitr.


Akizungumza na BINGWA jana, Katibu Mkuu wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa, alisema kuwa, wameandaa surprise kwa kuwaalika wanachama vigogo, akiwamo Mwenyekiti aliyejiuzulu.


“Kazi yangu ni kuwaalika wanachama wote kuhudhuria mkutano huu, hivyo na Mwenyekiti naye ni mwanachama, anaruhusiwa kuhudhuria bila pingamizi lolote,” alisema.


Alisema pia wamepanga kuandaa barua maalumu za mwaliko kwa Serikali, ikiwamo Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, chini ya Waziri wake, Harrison Mwakyembe.


“Kuanzia leo nitaanza kuandaa hizo barua kwa sababu mkutano ni wiki ijayo, lazima tualike upande wa watu wa serikali kwa kuwa hatuwezi kufanya kitu bila baraka zao,” alisema.


Mkutano huo maalumu kwa wanachama, umeitishwa ili kujadili masuala mbalimbali ya klabu hiyo, ikiwa pamoja na suala zima la mabadiliko ya kimfumo wa uendeshaji wa klabu.


Ikumbukwe Yanga imekuwa chini ya Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga, kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti, Yussuf Manji, Mei mwaka jana.


Mapema mwaka jana, Manji alikuja na mpango wa kutaka kujikodisha klabu kupitia kampuni aliyoisajili kwa jina la Yanga Yetu, lakini ukapata upinzani mkali na kuamua kuachana nao.