HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 5 Juni 2018

Chadema kutoshiriki uchaguzi ndogo kigoma


Pamoja na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupoteza Mbunge wake Mhe. Kasuku Samson Bilago, kimesema hakitashiriki uchaguzi mdogo kwenye jimbo la Buyungu mkoani Kigoma mpaka katiba mpya ya nchi itakapoandikwa.


Habari za uhakika zinaeleza Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amewaeleza wanachama wa chama hicho huko Kigoma na kusisitiza bila katiba mpya, CHADEMA kisitegemee kushinda uchaguzi wowote na huenda kikafa.


Amesema CHADEMA kinaelekea kupoteza matumaini yake kisiasa kutokana na kuwepo kwa mazingira aliyoyaita onevu na kandamizi ya kisheria, huku kiongozi huyo akisahau wamepata viti vya ubunge chini ya sheria zilizopo na katiba iliyoandikwa mwaka 1977.


"Pamoja na kwamba mwaka 2015 CHADEMA kimeshinda majimbo kadhaa, kupata kura za Urais karibu milioni 8, katiba iliopo bado ina utata na kuwapendelea watawala, hatushiriki uchaguzi mdogo wala uchaguzi mkuu ujao " Alisema Mbowe.


Alisema wameshiriki uchaguzi mdogo jimbo la Kinondoni na Siha wamekumbana na misukosuko, mikwara, vitisho na hekaheka ambazo baadhi yake hadi sasa zimewagharimu viongozi wa juu wa CHADEMA kwa kujikuta wakibambikiwa kesi.


Alipoulizwa haoni kama kukataa kwa CHADEMA kushirki ni kutokana na utendaji wa Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli kukubalika na Wananchi huku wafuasi wake wengi wakirudi CCM, alikana na kusema CCM inanunua wanachama na haiwezi kucheza soka kwenye uwanja usio na makorongo kwani kimezoea kucheza pekupeku kwenye mbigiri.


"Tunataka uwanja wenye majani na ambao umechongwa kwa greda la haki na kuwa tambarare kisheria na kikatiba. Hatutaki tubebwe na CCM isitake kushinda kiushikaji au kufanya vitisho vyake "Alisisitiza .


Alipotaliwa kujibu iwapo yupo tayari katiba ya CHADEMA ifanyiwe marekebisho kabla ya uchaguzi mkuu ujao kufanyika pia kutakiwa ajibu ikiwa atagombea au la, alidai hawezi kujibu swali la mwaandishi uchwara anayetetea mkate kwa CCM .


Je, CHADEMA kitashikiria msimamo wake wa kutoshiriki uchaguzi mdogo au kinaweka mikwara na mwisho wa siku watakuwa vigeugeu kwa kushiriki kama walivyogoma na kisha kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Siha na Kinondoni? ....