Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu, Wilfred Kidao, limesema kuwa linasubiria majibu ya CAF kuhusiana na ushiriki wa Mtibwa Sugar katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mtibwa wanasubiria hatima yao ya ushiriki baada ya kifungo cha miaka mitatu kufutia kushindwa kujikimu kusafiri kuelekea nje ya nchi ili kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakati ikiwa bingwa wa ligi, mwaka 2000.
Kidao amesema kuwa tayari walishatuma barua ya kuelekea CAF wakitaka kujua kama Mtibwa inaweza ikashiriki mashindano hayo baada ya adhabu ya miaka mitatu waliyokuwa wamefungiwa kumalizika.
Mtibwa Sugar bado hawana uhakika wa kushiriki mashindano hayo baada ya kupata nafasi kutokana na ushindi walioupata wa mabao 3-2 dhidi ya Singida United kwenye mchezo wa unaomtoa mwakilishi wa mashindano hayo ya Azam Sports Federation Cup (ASFC), mchezo uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid June 02 mwaka huu.