HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumapili, 10 Juni 2018

Manji Ndo mwenyekiti Yanga

Wanachama wa klabu ya Yanga, kwa kauli moja wamekataa kuridhia barua ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wao Yusuph Manji.

Manji alitangaza kujizulu nafasi yake May 23, 2017 na tangu wakati huo nafasi hiyo imekuwa ikikaimiwa na Makamu Mwenyekiti Clement Sanga.

Hata hivyo tangu wakati huo, barua ya Manji haikuwa imewahi kujadiliwa kwenye Mkutano Mkuu na kupewa baraka za Wanachama.

Kwa uamuzi huo wa Wanachama inamaanisha Manji bado anatambuliwa kama Mwenyekiti halali wa Yanga hadi pale utakapofanyika uchaguzi mwingine.

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga ameahirisha Mkutano huo na anampelekea ujumbe Manji kumwambia wanachama wa klabu ya Yanga wamegoma kujiuzulu kwake na bado wanamtambua kama Mwenyekiti wao.