Mwanachama maarufu Jitu Omari leo ameonja joto ya jiwe baada ya kutimuliwa ndani ya ukumbi unapofanyika Mkutano Mkuu wa Yanga, Masaki jijini Dar es salaam.
Jitu ni miongoni mwa Wanachama waliokuwa wakipinga kufanyika kwa Mkutano huo. Yeye anadaiwa kwenda Mahakamani kujaribu kuzuia Mkutano usifanyike
Maafisa wa jeshi la Polisi ilibidi wampe msaada wa ulinzi na kumtoa nje ya ukumbi baada ya wanachama kutaka kumpiga.
Mkutano huo tayari umeanza ambapo mgeni rasmi ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe, ambapo naye pia tayari ameshawasili.