HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Ijumaa, 1 Juni 2018

Yanga kusajiri wawiki kutoka Tanzania Prisons

Washambuliaji wawili wa Tanzania Prisons, Mohammed Rashid na Eliuter Mpepo wako kwenye mazungumzo ya kusajiliwa Yanga, imefahamika.

Rashid amekuwa akifuatiliwa na Yanga tangu wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi Novemba mwaka jana.

Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao 10 katika msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom uliomalizika, pia anawaniwa na Simba.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amethibitisha kuwa na mazungumzo na wachezaji hao lakini akasisitiza kuwa mazungumzo hayo ni ya awali.

Yanga imekuwa na mapungufu kwenye safu yake ya ushambuliaji msimu uliomalizika ilimtegemea Obrey Chirwa pekee ambaye naye hatma yake haijafahamika kwa kuwa mkataba wake unamalizika mwishoni mwa mwezi huu.