Mshambuliaji wa Njombe Mji Nitram Nchimbi amesema yuko tayari kujiunga na timu yoyote itakayofika nae makubalino ya kumsajili.
Baada ya Njombe Mji kuteremka daraja, mshambuliaji huyo anayehusishwa na Yanga amesema uongozi wa timu hiyo utamruhusu aondoke.
Bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo ya mkoani Njombe
Nchimbi aliifungia Njombe Mji mabao manne na kutengeneza mengine matano kwenye msimu wa ligi kuu ya Vodacom uliomalizika.
Ni miongoni mwa wachezaji 30 walioteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa VPL msimu huu.
Kama Yanga itafanikiwa kunasa sahihi yake, hakuna shaka ataweza kuimarisha safu ya ushambuliaji iliyoyumba msimu huu kutokana na majeruhi.