NA MWANDISHI WETU
YANGA wamefanya umafia nchini Kenya baada ya kumteka winga wa Kakamega Home Boys, Eston Esiye, usiku wa manane akiwa kambini na timu yake hiyo na kufanya naye mazungumzo kwa ajili ya kumsajili.
Aliyefanya umafia huo ni Mwenyekiti wa mashindano wa klabu hiyo, Hussein Nyika, ambaye pia anahusika sana na usajili na taarifa zinadai kuwa mazungumzo hayo yalikwenda vizuri.
Nyika na benchi la ufundi la Yanga walivutiwa na winga huyo baada ya kuonyesha uwezo mkubwa timu hizo zilipokutana mchezo wao wa ufunguzi wa michuano ya Sportpesa inayoendelea nchini Kenya.
Katika mchezo huo, Yanga walikubali kichapo cha mabao 3-1 na kutupwa nje ya michuano hiyo, lakini wamesema wasiondoke bure na badala yake wakaamua kumvamia winga huyo na kufanya naye mazungumzo ili kumsajili.
Taarifa zisizo na shaka zinadai Nyika aliwasiliana na mchezaji huyo wakakubaliana wakutane Hoteli ya Water Buck na baada ya kukutana mazungumzo yao yakafanyika.
“Ni kweli jamaa walikutana juzi usiku na kufanya mazungumzo ya kina, ilikuwa ni baada ya kumwona amecheza vizuri kwenye mchezo ambao timu hizo zilikutana Jumapili iliyopita,” alisema…..