HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 16 Desemba 2017

USAJIRI LIGI KUU TANZANIA BARA,SIMBA YA SAJIRI WATATU,YANGA 2,SINGIDA 7 MBEYA CITY......MAVUGO,GYAN OUT SIMBA......


USAJIRI LIGI KUU TANZANIA BARA,SIMBA YA SAJIRI WATATU,YANGA 2,SINGIDA 7 MBEYA CITY......MAVUGO,GYAN OUT SIMBA......

Simba imesajili wachezaji watatu wapya wa kigeni, beki Mghana Asante Kwasi, kiungo mshambuliaji Mzambia Jonas Sakuwaha na mshambuliaji Antonio Dayo Domingues kutoka Msumbiji.

Wakati dirisha dogo la usajili linakaribia kufungwa jana, viongozi wa Simba walikuwa wanahaha kukamilisha usajili huo, hususan wa mchezaji Kwasi, ambaye bado ana mkataba na klabu yake ya sasa, Lipuli ya Iringa.

Lakini kwa Sakuwaha na Domingues hakukuwa na tatizo na habari zinasema wachezaji hao watachukua nafasi za beki Mzimbabwe, Method Mwanjali na washambuliaji, Mghana Nicholas Gyan na Mrundi Laudit Mavugo. 

Yanga wamesajili wachezaji wawili tu wapya, beki Fiston 'Festo' Kayembe Kanku kutoka Balende FC ya DRC na mshambuliaji kinda, Yohanna Nkomola ambaye ni mchezaji huru, aliyekuwamo kwenye kikosi cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.

Azam FC imeingiza mmoja tu mpya, mshambuliaji Bernard Arthur kutoa Liberty Professional ya Ghana, baada ya kumuacha Mghana mwenzake, Yahya Mohammed.

Singida United imesajili saba wapya; Lubinda Mundia kwa mkopo kutoka Res Arrows ya Zambia, Daniel Lyanga kutoka Fanja ya Oman, Kambale Salita 'Papy Kambale' kutoka Etincelles ya Rwanda, Issa Makamba, Assad Juma, Ally Ng'azi na Mohamed Abdallah wote huru waliokuwa Sereneti Boys

Singida imewaacha wawili, Atupele Green na Pastory Athanas waliovunjiwa mikataba wakati Mohamed Titi na Frank Zakaria wametolewa kwa mkopo Stand United.

Mbeya City imewasajili George Mpole kutoka Majimaji na Abubakar Shaaban huru, baada ya kuwaacha Emmanuel Kakuti na mkongwe Mrisho Ngassa anayehamia Ndanda FC.

Kwa hisani ya Bin Zubeiry