HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Alhamisi, 19 Aprili 2018

Arafat kusajiriwa na Yanga

Jana baada ya mchezo dhidi ya Wolaitta Dicha, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga Hussein Nyika alifanya mazungumzo na mshambuliaji wa Dicha Djako Arafat.

Arafat ndiye aliyefunga bao pekee la Dicha kwenye dakika ya pili.

Mbali ya kuitumikia Dicha aliyojiunga nayo mwaka 2016, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amewahi kuichezea Anzhi Makhachkala inayoshiriki ligi kuu nchini Urusi.

Pia amewahi kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Togo kwa nyakati tofauti.

Yanga itakuwa na nafasi ya kuimarisha kikosi chake kabla ya kuanza hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho.