HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumapili, 8 Aprili 2018

Bayern Munich Yabeba Kombe la Bundesliga mbele ya Augsburg

Bayern Munich Yabeba Kombe la Bundesliga mbele ya Augsburg


Klabu ya soka ya Bayern Munich imetwaa taji la Bundesliga msimu wa 2018/19 baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Augsburg kwenye mchezo uliomalizika jioni hii.

 Bayern sasa imeweka rekodi ya kutwaa taji hilo mara 6 mfululizo huku msimu huu wakiwa wamechukua zikiwa zimebaki mechi 5 kabla ya ligi hiyo kumalizika. Baada ya ushindi wa leo wamefikisha alama 72 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine.

Bayern ambayo i[po chini ya kocha wa muda na aliyewahi kuipa mataji matatu (Trebble)  Jupp Heynckes, ilianza vibaya msimu chini ya kocha Carlo Ancelotti ambaye baadae alitimuliwa na kurejeshwa kwa Jupp na kila kitu kilibadilika kuanzia hapo.

Mabingwa hao wapya wa Bundesliga leo waliwapumzisha nyota wao Robert Lewandowski, Thomas Muller, Thiago Alcantala, Franck Ribery, Mats Hummels na Javi Martinez ambao wote walianzia kwenye benchi ikiwa ni sehemu ya mipango ya mechi ya UEFA jumanne ijayo dhidi ya Sevilla.

Tangu msimu wa 2012/13 Bayern haijapoteza taji hilo na imekuwa ikichukua bila ushindani mkubwa haswa baada ya mpinzani wake Borussia Dortmund kutokuwa kwenye kiwango kizuri misimu ya hivi karibuni.