HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 14 Aprili 2018

Breaking: Polisi Wadaiwa Kupigana Risasi Tanga, Mmoja Afariki Dunia



ASKARI Polisi waliokuwa lindoni katikaBenki ya CRDB Tawi la Tanga Mjiniwanadaiwa kupigana risasi leo Jumamosi, Aprili 14, 2018 na kusababisha kifo cha mwenzao mmoja, hata hivyo, majina yao hayajafahamika mara moja.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, inadaiwa kwamba, mmoja wa askari hao alimpiga risasi mwenzake na kumjeruhi mguuni hivyo akawa kama amepagawa na kuanza kufyatua risasi hovyo. Inadaiwa pia kwamba chanzo cha ugomvi huo ni tuhuma za wivu wa mapenzi.
Wakati tukio hilo likitokea inadaiwa askari wengine walikuwa eneo la jilani wakifanya mazoezi hivyo baada ya kuona mtu akirusha risasi hovyo walihisi ni mhalifu hivyo wakamfyatulia risasi iliyompata kichwani na kupoteza maisha