Breaking:AJALI MBAYA...FUSO LAGONGANA NA GARI NDOGO NA KUUA KAHAMA
Habari ziloizotufikia hivi punde zinasema ajali mbaya ya gari imetokea usiku wa kuamkia leo April 17,2018 mjini Kahama barabara kuu iendayo Rwanda karibu kabisa na kiwanda cha Ndegesera,ajali hiyo imehusisha gari aina ya Fuso yenye namba T453 AUM
na gari ndogo aina ya Vorkswagen yenye namba T819 DFK ambapo dereva wa fuso akijaribu kuovateki lori lililokuwa mbele yake aliligonga gari dogo kisha gari ndogo kutumbukia mtaroni na kuua abiria watatu wakiwemo watoto wawili na dereva wa gari hilo pia abiria wawili kujeruhiwa vibaya.
Taarifa zaidi zitakujia hivi punde...