HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 28 Aprili 2018

Edo Kumwembe atabilia simba ushindi

Mchambuzi nguli wa soka nchini Edo Kumwembe ameweka wazi kuwa timu anayoipa nafasi ya kushinda pambano la watani wa Jadi ni Simba, kutokana na aina ya wachezaji alionao msimu huu.

Akitoa utabiri wake kwenye mchezo huo leo ndani ya kipindi cha 'Shabiki On Saturday' cha East Africa TV,  Edo amesema nafasi kubwa ipo kwa Simba. Ameeleza Simba imekuwa bora msimu huu ukizingatia haijapoteza mchezo hata mmoja.

''Mimi nawapa Simba 'Advantage' ya kushinda pambano la kesho kutokana na wachezaji wao watatu Okwi, Kichuya na Bocco ambao wako kwenye kiwango cha juu zaidi msimu huu hivyo wanaweza kuamua matokeo ya ushindi wa Simba,'' amesema.

Kwa upande mwingine Edo amesema pamoja na Simba kuwa na nafasi kubwa lakini wasisahau mpira unadunda. Pia ameongeza kuwa hata misimu kadhaa Yanga amewahi kuwa kwenye ubora lakini Simba walishinda kwahiyo lolote linaweza kutokea.

Timu zote mbili zilikuwa zimeweka kambi mkoani Morogoro na zinatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam muda wowote jioni hii tayari kwa mchezo wa kesho ambao utaamua nani anakwenda kutwaa ubingwa.