Kwa mda mrefu kumekuwa na sheria ya mitandao ambayo inasimamia maudhui ya mitandao ya kijamii, ili kila mtu atumie bila kuvunja sheria au kuvuka mipaka
Pia tumeshuhudia sheria hii ikiwatia hatiani watu wengi huku wengine wakienda jela na wengine wakilipa faini mahakamani, lakini kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii vibaya lakini hawakamatwi wala kuchukuliwa hatua yoyote
Mmoja wapo ni huyu kijana anayejiita James delicious, ambaye amekuwa akitumia ukurasa wake wa Instagram kutukana watu matusi mazito ambayo ni ushahidi tosha kuwa mtu huyu anastahili kukamatwa mara moja kwani amekuwa akiwadhalilisha wanaume wenzake na wanawake pia amekuwa akitudhalilisha kwa kutukana matusi hadharani tena kwa kujiamini kama vile sheria haipo.
Kijana huyu amekuwa akitumia vibaya ukurasa wake kwa kuweka picha zisizo na maadili na kujitangaza hadharani kuwa ni shoga kitu ambacho ni kinyume na taratibu zetu
Nawasihi jeshi la Polisi kwa kushirikiana na TCRA huyu kijana anastaili kuwa jela mda mrefu tu lakini kutokana na kumuachia afanye anachotaka, ndio mnazidi kumpa kiburi, naomba serikali imulike kwa jicho la pili kwani matusi na maudhui ya kishoga anayopromote kwenye mitandao hapaswi kuwa uraiani hadi sasa