Kikosi cha Yanga jana kimefanya mazoezi Old Stadium mji wa Awassa kujiandaa na mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi wenyeji wao Wolaitta Dicha.
Yanga imewasili katika mji huo jana. Mchezo dhidi ya Dicha utapigwa dimbani hapo keshokutwa Jumatano, April 18 2018.
Huku ikiwa tayari inaongoza kwa mabao 2-0 ushindi iliyopata katika mchezo wa kwanza uliopigwa April 07 kwenye uwanja wa Taifa, Yanga inahitaji matokeo ya sare au ushindi ili kutinga hatua ya makundi.
Hata ikifungwa kwa bao 1-0 Yanga bado itatinga hatua ya