HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 10 Aprili 2018

Maandamano ya mange kimambi ni balaa yatua bungeni

Maandamano ya mange kimambi ni balaa yatua bungeni


WAKATI ikiwa zimebaki siku 16 kufikia Aprili 26 mwaka ambapo itakuwa siku ya  Maandamano ambayo yameandaliwa na Mwanaharakati Maarufu kwenye Mitandao ya Kijamii,Mange Kimambi,

Maandamano hayo yametinga Bungeni Dodoma baada ya  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Waprili 26 lemavu, Jenista Mhagama kufunguka na kutoa ushauri kuhusu suala la maandamano na kusema kuwa mtu yoyote ambaye ana ratibu maandamano lazima afuate sheria hata kama maandamano yanatambulika kikatiba.

Jenista Mhagama amesema hayo bungeni na kudai kama kila mtu ataamua kuandamana kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu hilo litakuwa jambo ambalo si sawa hivyo amevitaka vyama vya siasa kufuata sheria za nchi na si kuvunja sheria za nchi.

"Suala la maandamano katika nchi yetu ya Tanzania linaratibiwa na sheria za usalama ndani ya nchi chini ya vyombo vya usalama hasa polisi na Katiba haiwezi kuchukuliwa kwamba ni kigezo cha kuviruhusu vyama kufanya maandamano bila kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa.

"Ninaomba sana Watanzania wote na niviombe vyama vyote vya siasa katika nchi yetu ya Tanzania wahakikishe wanazingatia sheria. 

"Katiba yetu imeruhusu maandamano lakini maandamano yameratibiwa kisheria na kama yameratibiwa kisheria lazima tuhakikishe kwamba tunazingatia sheria katika kuratibu maandamano nchini kwetu Tanzania"

Jenista Mhagama aliendelea kutoa maelezo kuhusu masuala ya maandamano

"Labda niulize swali moja tukiamka hapa siku moja asubuhi na kila mtu ameamua kuandamana wakulima, wafanyakazi yaani kila mtu aamue tu kuandamana kwa sababu tu Katiba imesema nadhani itakuwa siyo sawa na nichukue nafasi hii kuviomba vyama vya siasa kuheshimu Katiba na sheria katika kutekeleza wajibu wao na siyo kuvunja sheria za nchi yetu Tanzania"