HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 9 Aprili 2018

MFUNGWA KWA SIKU ANATUMIA SHILINGI 1,324 KWA CHAKULA

MFUNGWA KWA SIKU ANATUMIA SHILINGI 1,324 KWA CHAKULA

Naibu Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Hamad Masauni amelieleza Bunge kuwa gharama ya kuhudumia chakula kwa mfungwa mmoja kwa siku ni wastani wa Tshs. 1,342.
Vilevile ameeleza kuwa serikali imeendelea kuboresha huduma za wafungwa na mahabusu magerezani kwa kununua vifaa mbalimbali na inapotokea wafungwa kulala bila blanketi, shuka au neti sio sehemu ya adhabu bali inatokana na idadi kubwa ya wafungwa katika gereza husika.

Akitoa ufafanuzi zaidi Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba ameeleza siyo kila gereza nchini lina msongamano bali msongamano magerezani hutokana na kukithiri uhalifu katika mkoa husika.

Waziri Nchemba ameliambia Bunge kuwa katika mikoa ya Lindi baadhi ya magereza yamekuwa na wafungwa na mahabusu wachache pamoja na magereza ambayo yapo katika baadhi ya wilaya za mkoa wa Tanga.

#KutokaBungeni