Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema baada ya kutambulishwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo kuwa ni rafiki yake katika Ibada ya kusimikwa Mhashamu Isaack Amani kuwa Askofu Mkuu Jimbo la Katoliki la Arusha.
Mbunge huyo wa Arusha hajasita ameweka wazi jinsi alivyotambulishwa na Mbunge huyo kuwa, RC Gambo hakuogopa muongo madhabahuni kwa kumtambulisha kuwa ni rafiki yake.
“Ktk Ibada ya kusimikwa Askofu,Mh Rais aliongea neno la Mungu kuhusu Amani na Haki.Bila shaka demokrasia na haki vitashamiri tena.Askofu Amani yeye akasisitiza ushirikiano kisiasa bila kubaguana.Mrisho Gambo(RC) yeye akuogopa kuwa muongo madhabauni, eti aliniita Mimi rafiki yake,” ameandika Lema kwenye ukurasa wake wa Twitter.