Mhasibu wa Manispaa ya Dodoma, Charles Gongwe amekutwa amefariki kwa kujinyonga nyumbani kwake eneo la Area C, Kata ya Kiwanja cha Ndege mjini Dodoma. Ofisa Habari wa Manispaa ya Dodoma, Ramadhani Juma amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema uchunguzi bado unaendelea.