HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 9 Aprili 2018

Spika wa Bunge aungana Mbunge wa Upinzani(CHADEMA)

Spika wa Bunge, Job Ndugai amewashauri Wabunge wanawake kuungana na kupeleka hoja ya kuwasaidia kina mama wanaoteseka magereza kwa kufungwa kwa madeni madogo madogo huku wakiwa na watoto na wenye maradhi ambao serikali inapaswa kuwagharamia kila siku
Spika Ndugai ametoa ushauri huo baada ya Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko kuhoji, kwanini serikali isitumie busara zaidi kwa wafungwa hususani wakina mama wenye watoto wachanga ambao wanafungwa kwa kesi za kudaiwa laki 1-2 halafu wanafungwa miezi 6 kwa maana wanakuwa wanaenda kutumia gharama kubwa kuliko deni wanalodaiwa.
Hata hivyo swali la Esther Matiko lilijibiwa na William Tate Ole -Nasha amesema suala hilo ni la kisheria hivy kama Mbunge huyo ameona sheria hiyo imepitwa na wakati na haitendi haki anapaswa kupeleka hoja ya sheria bungeni ili iweze kubadilishwa.
Naye Spika Ndugai ameongeza "Na kwa kweli wabunge wanawake mpo wengi hapa kama mambo hayo yapo kweli mnapaswa kuungani ili kuangalia mateso ya kina mama wa aina hiyo"