HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 23 Aprili 2018

Msemaji wa klabu ya Lipuli FC Clement Sanga amesema bado klabu hiyo haijapokea taarifa rasmi juu ya mshambuliaji wao Adam Salamba kusajiliwa na Yanga.

Yanga ina nafasi ya kusajili mchezaji mmoja kukamilisha idadi ya wachezaji 30 kabla ya kuanza kwa hatua ya makundi michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika May 04.

Salamba ana sifa sahihi za kuweza kuongezwa kwenye kikosi cha Yanga ambacho kwa hakika kina mapungufu kwenye safu ya ushambuliaji kutokana na kuwakosa Donald Ngoma na Amissi Tambwe.

Kama Yanga itafanikiwa kumpata, ataongeza makali ya safu yake ya ushambuliaji mara dufu.

Pia sio jambo zuri kwa Yanga kuingia kwenye michuano hiyo ikiwa na mshambuliaji mmoja wa asili.

May 04 Yanga itakuwa ugenini nchini Algeria kucheza mchezo wa kwanza hatua ya makundi dhidi ya USM Alger.

Tayari dirisha la usajili la CAF limefunguliwa kwa timu ambazo awali zilituma wachezaji chini ya 30.

Kanuni zinaeleza, wiki mbili kabla ya kuanza hatua ya makundi, timu zenye wachezaji pungufu ya 30 zinaweza kusajili hadi wachezaji saba (kulingana na upungufu uliopo).

Mwisho wa zoezi hilo ni August 05.