HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Alhamisi, 12 Aprili 2018

Mtibwa Sugar yaitwanga Ndanda 1-

Mtibwa Sugar yaitwanga Ndanda 1-

Mtibwa Sugar imefanikiwa kuibuka na ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Manungu leo.

Kikosi hicho kimejipatia bao lake kupitia kwa Kelvin Sabato aliyefunga katika dakika ya 22 ya kipindi cha kwanza.

Wakata miwa hao wa Morogoro wamepata matokeo baada ya kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Simba kwa kichapo cha bao 1-0.

Mtibwa sasa imefikisha jumla ya alama 33 kwenye msimamo wa ligi huku ikicheza michezo 23 na ikiwa nafasi ya 6.

Wakati huo Ndanda FC imekamata nafasi ya 12 ikijikusanyia alama 23 huku ikicheza jumla ya mechi 24 msimu huu.

Mechi nyingine ambayo ilipaswa kupigwa Uwanja wa Mabatini leo ilikuwa ni kati ya Ruvu Shooting FC dhidi ya Azam FC.

Mtanange huo umeahirishwa kutokana na mvua kubwa kunyesha huku ikisababisha Uwanja wa Mabatini kujaa maji.